Yanga inapumulia mashine CAF

Yanga inapumulia mashine CAF

NA ISMAIL KHAMIS
WAPENZI wa soka tumeshuhudia mchezo wa matumaini kwa Yanga ambao ungempa asilimia kubwa ya kusonga alipoteza dhidi ya timu ya Farrabat.
Mechi ambayo klabu hiyo ilikuwa nyumbani kwake iliibuka kidedea kwa bao 1-0.
Swali ni je, yapo matumaini ya Yanga kusonga mbele? Jibu ni ndiyo ingawa kwa mbinde.
Hadi sasa klabu iliyojihakikishia kufuzu kwenye kundi la Yanga ni Al Ahaly ya Misri.
Mechi pekee ambayo itaamua nani anaunga naye itaamuliwa na ushindi wa mechi kati ya Yanga dhidi ya kibonde Kabylie au Far Rabati apate kipigo kutoka kwa Al ahaly.

Ahaly vs Far Rabat
Yanga Vs Kabylie

Hizo mechi ni muhimu sana kuamua nani kati ya Yanga na Far Rabat ataungana na Al Ahaly ambaye tayari ameshatangulia mazima.

1. Far Rabat yeye anachohitaji sare pekee au ikitokea akafungwa basi mechi ya  Yanga huko Zanzibar ashinde sio chini ya goli mbili bila.
2. Yanga anahitaji ushindi tena mnono pale Zanzibar.

Kwa nini?
Katika mashindano haya ya CAF Champion League kitakachokubeba ni.

Iwapo pointi zitakuwa sawa kitachachoangaliwa ni Mechi mlizokutana, Na nani alipigwa goli nyingi.
Nani alizuia kupigwa goli nyingi

Kwa matokeo ya Yanga kupoteza kipengele cha kukutana tayari kimelingana kwa hiyo wataenda kingine.
Hadi sasa yanga ana GD ya negative mbili (-2) huku Far Rabat ana positive moja (+1)
Kwa hiyo hapo yanga inabidi ashinde goli za kutosha kule Zanzibar ili afute hiyo negative mbili (-2) na aingie positive na pia wakati huohuo amuombee Far rabat afungwe pale Cairo idadi ya goli zisizopungua tatu zitakazoipelekea ipoteze ile positive yake na kuingia zero hadi negative.
Kwa hiyo hapo huwezi kadilia hata idadi ya ushindi wa hao jamaa.

Kwa mfano
Yanga akishinda 1
Far akafungwa 3
Yanga anafuzu maana atakuwa amepunguza negative 2 hadi -1.. huku kitendo cha Far kufungwa 3 atakuwa amefuta ile positive yake 1 na kujiwekea negative 2. Kwa hiyo game za mwisho ndo zitaamua.

You may also like

Ulaji vyakula vya viwandani chanzo cha magonjwa yasiyoambukiza

Ulaji vyakula vya viwandan...

Simba kicheko Katiba mpya

Simba kicheko Katiba mpya

Maneno afichua siri Kliniki ya bure

Maneno afichua siri Kliniki...

GAZETI LA WATANZANIA 19/02/2026

GAZETI LA WATANZANIA 19/02/...